Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani), wakati alipowasilisha Utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2022/23 na Mipango ya Utekelezaji kwa mwaka 2023/24 ya Sekta ya Uchukuzi, jijini Dodoma.
Muonekano wa barabara ya Kabingo-Kasulu-Manyovu yenye urefu wa kilometa 260.6 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Kigoma.
Muonekano wa hatua meli ya MT. Sangara ambayo inakarabatiwa na Kampuni ya KTIMI ya Nchini Korea Kusini kwa gharama ya shilingi takribani bilioni 8 na ukarabati huo umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika mwezi aprili mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) iliyotengewa fedha kwa mwaka wa Fedha 2022/23, kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Sekta ya Uchukuzi, wakimsikiliza Katibu Mkuu Bw.Gabriel Migire (hayupo pichani) wakati akifunga baraza la wafanyakazi, lililofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uchukuzi, ambaye ni Katibu Mkuu-Uchukuzi, Bw.Gabriel Migire, akizungumza na wajumbe wa baraza (hawapo pichani) wakati akifunga baraza la wafanyakazi Sekta ya Uchukuzi, lililofanyika Jijini Dodoma.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha (km 19.2), jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 98 na unatarajia kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi April, 2023.
Baadhi ya Wajumbe wa Sekta ya Uchukuzi, wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi, lililofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akiwa na Mbunge wa Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa, wakishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Nyamwage hadi Utete (km 33.7) kwa kiwango cha lami kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya China Railway Seventh Group, wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Muonekano wa Bandari ya Karema baada ya ujenzi wake kukamilika. Ujenzi wa Bandari hiyo umegharimu takribani bilioni 47.9 na inatarajiwa kuhudumia mzigo mkubwa unaozalishwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya mwendo kasi awamu ya pili inayoshia Mbagala.
Mtaalam wa mitambo Christian Kabundungulu, akifafanua namna magurudumu ya treni yanavyochongwa kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) hawapo pichani, wakati Kamati hiyo ilipotembelea karakana hiyo Mkoani Tabora.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa, Mhandisi Daniel Kindole akielezea maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha Iringa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe Selemani Kakoso na Wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani), wakati walipotembelea na kukagua Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Kichwa cha Treni ya kawaida-MGR cha kuvutia mabehewa ya abiria na mizigo kwa njia kuu aina ya 88 class kikifanyiwa ukarabati ndani ya Karakana ya Ukarabati wa Vichwa vya Treni ya kawaida-MGR Mkoani Morogoro
Kaimu Katibu Mkuu-Sekta ya Ujenzi, (wa tatu kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Sekta ya Ujenzi, mara baada ya kufungua semina ya mafunzo ya masuala ya afya, yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu-Sekta ya Ujenzi, Bi Saumu Mruke, akifanya vipimo vya afya kuhamasisha upimaji wa afya kwa hiyari kwa watumishi wa Sekta hiyo mara baada ya ufunguzi wa Semina ya Masuala ya afya kwa watumishi wa Sekta hiyo, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Ludovick Nduhiye, akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wakipokea taarifa ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete, akisisitiza jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wakipokea taarifa ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), mkoani Morogoro.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu-Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour kuhusu utekelezaji wa maradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara, wakati kamati hiyo ilipokagua barabara ya Njombe-Moronga KM 53.9 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Waziri wa Miundombinu, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Nchini Zambia, Mhe. Mhandisi Charles Milupi (katikati), mara baada ya Waziri Prof. Mbarawa kuzungumza nae, mjini Lusaka.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani), wakati kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa SGR Sehemu ya Morogoro-Makutupora.
Katibu Mkuu (Uchukuzi), Gabriel Migire, akimsikiliza Mhe. Lt. Jen. Mathew Mkingule, Balozi wa Tanzania nchini Zambia baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kenneth Kaunda, Lusaka - Zambia kwa ajili ya kushiriki katika Kikao cha Bodi ya TAZARA.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Balozi Mhe. Lt. Jen. Mathew Mkingule, muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za TAZARA Jijini Lusaka, Zambia.
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akisisitiza jambo wakati wa kikao kilichowakutanisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na watendaji wa Wizara kujadili kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara Bungeni, jijini Dodoma.
Title | Tarehe | Pakua |
---|---|---|
TANGAZO LA KOZI MAALUM YA MAOPARETA WA MITAMBO YA KAZI ZA UJENZI (GRADER OPERATOR COURSE) | 2022-11-09 | Pakua |