Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

KADCO ONGEZENI UBUNIFU ILI KUVUTIA MASHIRIKA YA KIMATAIFA ZAIDI


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David kihenzile ameutaka Uongozi wa Kampuni ya Uendeshwaji na Uendelezwaji wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kilimanjaro(KADCO) ambao ndiyo waendeshaji wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kilimanjaro(KIA) kuongeza ubunifu ili kuvutia zaidi Mashirika ya Kimataifa.

 

Akizungumza Jijini Arusha wakati wa muendelezo wa ziara zake za kuongea na Viongozi na Kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo amesema mpaka Sasa KIA inahudumia Mashirika 13 ya Kimataifa Kiwango ambayo ni machache ukilinganisha na uwekezaji na jitihada mbalimbali za Kiserikali zilizofanyika.

 

"Kiongozi wetu mkuu Rais wa Awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaanza yeye mwenyewe kuigiza kwenye filamu ya Royal Tour ambapo alitua hapa ili kuvutia wageni zaidi Sasa ni wakati wa Kampuni kuwa na Mikakati ya Masoko inayoonekana, inayokunalika na inayotekelezeka ya kutafuta masoko nje ya Nchi ili kuvutia Mashirika ya Kimataifa zaidi" amesisitiza Kihenzile.

 

Mhe Kihenzile amesema uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Arusha upo eneo la kimkakati kwani Mkoa huo ni kitovu Cha utalii Kwa ukanda wa Kaskazini Kwa kuwa na vivutio bingo vya utalii pia  Kuna ushindani mkubwa wa kibiashara na Nchi  jirani hivyo kutoa Rai jitihada za dhati zifanyike kujitangaza Kimataifa ili kuunga mkono maono makubwa ya Rais ya kuifungua Nchi Kimataifa.

 

Amesema amefurahi kuona Maboresho ya Maeneo ya maegesho ya magari ambapo Sasa yanahidumia magari zaidi ya 120 ikiwa ni ongezeko la mara mbili zaidi ya ilivyokuwa awali, ukamilifu wa Maeneo ya kuhifadhia bidhaa ya ubaridi(Cold Rooms) sambamba na ukamilifu wa mindombinu ya kuingia uwanjani hapo ambavyo vitavutia watumishi zaidi hasa wakulima.

Pamoja na hayo ameutaka Uongozi wa  KADCO na Taasisi zote za Uchukuzi kuwa na utaratibu mzuri wa kutekeleza maelekezo ya viongozi wa  Serikali Kwa kuwa na mfumo wa ufuatiliaji na utekelezaji wa maelekezo hayo.

Kihenzile amesema yapo maagizo mengi hutolewa na viongozi mbalimbali ila utaratibu uliopo hivi Sasa hakuna ufuatiliaji makini wa maagizo hayo hivyo ameielekeza Kampuni ya Uendeshwaji na Uendelezwaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Arusha kuhakikisha inawasilisha Wizarani taarifa kamili ya maelekezo yote yaliyotolewa na Viongozi Mbalimbali wa Serikali  Kwa nyakati tofauti  na utekelezaji wake.

Akitoa salamu za utangulizi Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO ambao ndiyo waendeshaji wa KIA Bi Christine Mwakatobe  amesema  kiwanja hicho kilojengwa na Serikali na kuanza kutumika rasmi mwaka 1971 kikiwa na lengo la  kutoa Huduma Bora za Usafiri wa anga na kuimarisha shughuli za utalii Nchini.

Kuhusu mafanikio Bi Christine amesema Hali ya utendaji na shughuli mbalimbali za KIA kuanzia mwaka 2019 Hadi 2023 ni wa ufanisi mkubwa ambapo idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 794,337 mpaka 929,553, Mizigo kutoka kilo mil 3 mpaka Mil 4.3, idadi ya miruko kutoka 20,756 mpaka 22,715  huku mapato yakipanda kutoka Bil 26 mwaka 2019/2020 mpaka Bil 31.7 sawa na ongezeko la asilimia 59.

Kwa upande Mwingine Mhe Kihenzile alipata fursa ya kutembelea na Kukagua maendelea ya Maboresho mbalimbali na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Moshi uliopo poa Mkoani Kilimanjaro unaosimamiwa na TANROAD ambapo kinafanyika ujenzi wa njia mbili za miruko ya Ndege Kwa lami mita 1,200 na changalawe mita 1,400 utakaogharibu