Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Habari

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI (MSCL) KUJIENDESHA KIBIASHARA.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), kuhakikisha meli zote za kampuni hiyo zinafanya kazi na kujiendesha  kibiashara .

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Selemani Kakoso kwenye Kikao cha kupokea taarifa za utendaji kazi ya kampuni hiyo kwa kipindi cha Julai- Oktoba 2023.

“MSCL inatakiwa kuhakikisha inakarabati Meli zote na kusimamia meli zilizopo katika Ziwa Tanganyika, Ziwa nyasa na Ziwa Victoria na Mjiendeshe kibiashara” alisema Kakoso.

Pia Kakoso ameongeza kwa kusema kuwa katika bajeti ya Mwaka 2022/2023 MSCL ilitengewa shilingi Bilioni 124 hivyo kamati hiyo inamatumaini itasaidia Kampuni hiyo kuweza kukarabati na kujenga meli Mpya ili kuweza kutoa huduma ya Usafiri kwa Njia ya Maji.

Kwa Upande wake  Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma kwa njia ya Maji katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria na Tayari Serikali  imeshawezesha kusainiwa mikataba ya Ujenzi wa Meli mbili za Mizigo pamoja na Kiwanda cha kutengeneza Meli katika ziwa Tanganyika.

“ Serikali pamoja na kutoa fedha ya Ujenzi wa Meli Mpya mbili lakini pia serikali imetoa fedha ya ukarabati wa meli ya MV. Umoja, MV.Liemba na MV. Muongozo” alisema Kihenzile.

Mkurugenzi wa  MSCL Erick Hamis  amesema kuwa  Ujenzi wa Meli ya MV.Mwanza hapa kazi tu inatarajia kukamilika Mwezi Mei mwaka huu kwani hatua iliyofikia sasa ni uwekaji wa viti na Vitanda, na  vitu vyote kama Mashine na Mitambo vimekamilika.

MSCL inajumla ya meli 18 kati ya meli hizo meli saba tu ndio zinafanya kazi hivyo Kampuni hiyo inaendelea kusimamia na kuendesha meli hizo katika Ziwa  Nyasa,Ziwa Tanganyika na Victoria.